Sera ya Faragha
Imesasishwa: Oktoba 2026
Tunaheshimu faragha yako. Ukurasa huu unaeleza taarifa tunazokusanya, kwa nini, na unachoweza kufanya.
1. Taarifa tunazokusanya
Unapoingia kwa Google: jina lako, barua pepe na picha ya wasifu.
Unapojifunza: masomo uliyokamilisha, maendeleo yako na kozi ulizonunua.
Unapolipa: namba ya simu ya malipo na hali ya malipo (imefanikiwa, imeshindwa). Namba za siri za mitandao ya simu hatuzipati; zinabaki kwa mtoa huduma wa malipo.
Unapotuma maoni: ujumbe wako, ukurasa uliokuwepo na aina ya simu, ili tuweze kurekebisha tatizo. Namba ya WhatsApp au barua pepe ni hiari.
Takwimu za jumla za ukurasa wa kwanza (mfano mgeni amebonyeza kitufe cha kupakua), bila kukutambulisha jina.
2. Tunazitumiaje
Kukuingiza kwenye akaunti, kufungua kozi ulizolipia, kukumbuka ulipoishia, kuthibitisha malipo, kujibu maswali na maoni yako, na kuboresha App.
Hatuuzi taarifa zako kwa mtu yeyote.
3. Tunazishiriki na nani
Google, kwa ajili ya kuingia.
FimiPay, kwa ajili ya kuchakata malipo.
Cloudflare, ambayo inaendesha App na kuhifadhi data kwa usalama.
Tunaweza kutoa taarifa ikiwa sheria inatulazimisha.
4. Vidakuzi na hifadhi ya kifaa
Tunatumia kidakuzi cha kukuweka umeingia, na hifadhi ya kifaa kukumbuka mapendeleo kama mandhari ya giza au nyepesi.
Hatutumii vidakuzi vya matangazo.
5. Muda wa kuhifadhi
Tunahifadhi taarifa za akaunti na malipo kwa muda unaohitajika kukupa huduma na kutimiza mahitaji ya kisheria na hesabu za biashara.
Maoni yanahifadhiwa hadi tutakapoyashughulikia.
6. Haki zako
Unaweza kuomba kuona, kusahihisha au kufutiwa taarifa zako. Tuandikie WhatsApp na tutakusaidia.
Kufuta akaunti kunafuta ufikiaji wako wa kozi ulizolipia, isipokuwa pale tunaporuhusiwa au kulazimika kuhifadhi rekodi za malipo.
7. Usalama
Tunatumia muunganisho salama (HTTPS) na kulinda sehemu za usimamizi. Hakuna mfumo salama kwa asilimia mia moja, hivyo tunakushauri ulinde akaunti yako ya Google.
Una swali kuhusu ukurasa huu?