Rudi mwanzo

RAQIIMTECH

Sera ya Kurejeshewa Pesa

Imesasishwa: Oktoba 2026

Kozi zetu ni maudhui ya kidijitali yanayofunguka mara moja unapolipa. Hivi ndivyo tunavyoshughulikia matatizo ya malipo.

1. Jaribu kwanza bila kulipa

Kuna masomo ya bure ndani ya App. Yasome kabla ya kununua ili ujue ubora na mtindo wa kufundisha.

2. Tunarejesha pesa lini

Umelipa lakini kozi haikufunguka na hatukuweza kulitatua ndani ya siku 7 tangu ulipotujulisha.

Umelipa mara mbili kwa kozi ile ile (tunarudisha malipo ya ziada).

Kuna hitilafu ya kiufundi kwenye kozi iliyozuia kuitumia na hatukuweza kuirekebisha ndani ya siku 7.

3. Haturejeshi pesa lini

Umebadilisha mawazo baada ya kozi kufunguka na kuanza kuisoma.

Umenunua kozi isiyokufaa kwa kiwango chako, wakati masomo ya bure yalikuwepo kujaribu.

Ufikiaji umepotea kwa sababu ulimpa mtu mwingine akaunti yako.

4. Jinsi ya kuomba

Tuandikie WhatsApp ndani ya siku 7 tangu ulipolipa. Tuambie barua pepe uliyoingia nayo, kiasi ulicholipa, na tarehe.

Ukiwa na ujumbe wa muamala (SMS) kutoka kwa mtandao wako wa simu, tutumie, unatusaidia kuharakisha.

5. Muda wa kurejesha

Ombi likikubaliwa, tunarudisha pesa kwa namba ile ile ya simu uliyolipia, kwa kawaida ndani ya siku 7 za kazi. Ada za mtandao wa simu zinaweza kutofautiana.

Una swali kuhusu ukurasa huu?

Pakua App kwa hatua 3

  1. 1Gusa menu juu kulia kwenye kivinjari chako.
  2. 2Chagua Install app au Add to Home screen.
  3. 3Gusa Install. Ikoni ya RAQIIMTECH itaonekana kwenye skrini yako.

Hakuna ada ya kupakua. App ni nyepesi na haichukui nafasi kubwa kwenye simu.